Facebook Twitter Instagram Pinterest YouTube Tumblr LinkedIn RSS
    • About
    • Advertise
    • Contribute
    • Donate
    • Forum
    • Contact
    Login
    InfoStride NewsInfoStride News
    • Home
    • Business
    • Celebrity
    • Crime
    • Nigeria
    • Politics
    • Sports
    • Technology
    • More
      • COVID-19
      • Editor’s Picks
      • Health
      • Opinions
      • Press Releases
      • World
    Subscribe
    InfoStride NewsInfoStride News
    Home»News»African News»East African News»Shirika la ndege la flydubai limetangaza njia tatu nchini Tanzania

    Shirika la ndege la flydubai limetangaza njia tatu nchini Tanzania

    East African News By apofeedSep 25, 2014No Comments6 Mins Read
    Facebook Twitter WhatsApp Pinterest LinkedIn Tumblr Email Reddit VKontakte

    DAR ES SALAAM, Tanzania, September 23, 2014/African Press Organization (APO)/ — Shirika la ndege lenye makao yake Dubai leo limetangaza uzinduzi wa safari za ndege za Dar es Salaam, Zanzibar na Kilimanjaro nchini Tanzania. Safari za ndege za nchi hii ya Afrika Mashariki zitaanza Oktoba, zikikuza mtandao wa shirika hili la ndege barani Afrika hadi vituo 12.

    Logo: http://www.photos.apo-opa.com/plog-content/images/apo/logos/flydubai.jpg

    Photo 1: http://www.photos.apo-opa.com/index.php?level=picture&id=1388 (Ghaith Al Ghaith, Chief Executive Officer of flydubai)

    Photo 2: http://www.photos.apo-opa.com/index.php?level=picture&id=1297 (flydubai fleet)

    Photo 3: http://www.photos.apo-opa.com/index.php?level=picture&id=1389 (Sudhir Sreedharan, Senior Vice President Commercial (GCC, Subcontinent and Africa)

    Photo 4: http://www.photos.apo-opa.com/index.php?level=picture&id=1298 (flydubai Business Class)

    Photo 5: http://www.photos.apo-opa.com/index.php?level=picture&id=1387 (Economy seats)

    Photo 6: http://www.photos.apo-opa.com/index.php?level=picture&id=1295 (flydubai Business Class Lounge)

    Photo 7: http://www.photos.apo-opa.com/index.php?level=picture&id=1386 (Downtown Burj Khalifa)

    Akizungumzia kuhusu uzinduzi wa safari hizi, Ghaith Al Ghaith, Afisa Mkuu Mtendaji wa flydubai (http://www.flydubai.com), alisema: “Kwa kuongeza safari hizi tatu mpya nchini Tanzania tumekuza mtandao wetu mara mbili katika Afrika ya Kaskazini na Mashariki mwaka huu, tukiimarisha ahadi yetu ya kuhudumia masoko ambayo hayakuhudumiwa vya kutosha.”

    Hivi karibuni flydubai ilitangaza uzinduzi wa safari za ndege za Bunjumbura nchini Burundi, Entebbe nchini Uganda na Kigali nchini Rwanda na safari za vituo hivi zitaanza mwishoni mwa Septemba.

    Tanzania ni kitovu cha eneo upande wa utalii wa Afrika Mashariki na mwakani 2013 nchi hiyo iliwakaribisha watalii milioni 1. Kulingana na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), idadi hii inatarajiwa kuongezeka mara mbili na watalii milioni 2 wakitarajiwa ifikapo 2017.

    Makamu Mkuu wa Rais wa Biashara, Sudhir Sreedharan (GCC, Bara Dogo na Afrika), alisema, “Mtandao wetu unaoendelea kukua unaunga mkono Dira ya Utalii ya 2020 ya Dubai inayolenga kuwavutia wageni milioni 20 katika Umoja wa Falme za Kiarabu ifikapo 2020.

    Kwa kutoa huduma za kuaminika, kwa bei nafuu na zilizo rahisi za usafiri kutoka Tanzania, tunawapa abiria fursa ya kusafiri Dubai na kuunganisha safari zao na zaidi ya vituo 200 duniani kote kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai.”

    Tanzania ni nchi inayojulikana kwa uzuri wake wa asili na wanyamapori. Dar es Salaam ni kitovu cha biashara nchini Tanzania na mji huo una bandari linalovutia na vivutio tele vya kitamaduni na kihistoria. Unguja, inayojulikana kama Kisiwa cha Viungo, imefunikwa na pwani nyeupe na imejaa utamaduni, historia na wanyamapori wanaopatikana huko tu. Zaidi ya hayo, vilele vya Mlima Kilimanjaro vilivyofunikwa na theluji huwakaribisha watalii kwa matembezi na kuteleza juu ya theluji mwaka mzima.

    flydubai imeunda mtandao mpana barani Afrika ulio na safari za ndege za Addis Ababa nchini Uhabeshi, Alexandria nchini Misri, Khartoum na Port Sudan nchini Sudani, Djibouti mji mkuu wa Djibouti, Juba nchini Sudani Kusini pamoja na Bujumbura nchini Burundi, Entebbe nchini Uganda na Kigali nchini Rwanda.

    See also  SOUTH SUDAN: MSF BRIEFING ON WORSENING HUMANITARIAN CRISIS AND INADEQUATE AID RESPONSE

    Maelezo ya Safari za Ndege”

    Dar es Salaam

    flydubai itaendesha safari za ndege kila siku kati ya Dubai na Dar es Salaam kuanzia tarehe 16 Oktoba 2014.

    FZ670 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 6:20 machana saa za ndani, itue katika Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 12:55 jioni saa za ndani.

    FZ672/674 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 12:20 jioni saa za ndani, itue katika Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 7:00 usiku saa za ndani.

    FZ669/671/673 imepangiwa kuondoka Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 12:40 asubuhi saa za ndani, iwasili Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 5:20 asubuhi saa za ndani.

    Nauli za safari ya pande zote

    Nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Uchumi kutoka Dar es Salaam hadi Dubai itaanzia Dola 399 za Marekani ikijumuisha mzigo wa 20kg uliokaguliwa, huku nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Biashara itaanzia Dola 1,499 za Marekani na inajumuisha kodi zote na mzigo wa 40kg uliokaguliwa. Hizi ni nauli maalum za uzinduzi za mwezi mmoja.

    Kilimanjaro kupitia Dar Es Salaam

    flydubai itaendesha safari mbili za ndege kila wiki kati ya Kilimanjaro na Dubai kupitia Dar Es Salaam kuanzia tarehe 17 Oktoba 2014.

    Jumatatu na Ijumaa:

    FZ674 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro saa 10:10 jioni saa za ndani, itue Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 7:00 usiku saa za ndani na katizo la safari la saa moja mjini Dar es Salaam.

    FZ673 imepangiwa kuondoka Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 12:40 asubuhi saa za ndani, iwasili Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro saa 7:25 mchana saa za ndani na katizo la safari la saa moja mjini Dar es Salaam.

    Nauliza pande zote mbili

    Nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Uchumi kutoka Kilimanjaro hadi Dubai itaanzia Dola 399 za Marekani ikijumuisha mzigo wa 20kg uliokaguliwa, huku nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Biashara itaanzia Dola 1499 za Marekani na inajumuisha kodi zote na mzigo wa 40kg uliokaguliwa. Hizi ni nauli maalum za uzinduzi za mwezi mmoja.

    Zanzibar kupitia Dar Es Salaam

    flydubai itaendesha safari mbili za ndege kila wiki kati ya Unguja na Dubai kupitia Dar Es Salaam kuanzia tarehe 19 Oktoba 2014.

    See also  UN Special Representative for Somalia condemns violence in Baidoa

    Jumanne na Jumapili: FZ672 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Ndege wa Unguja saa 9:40 mchana saa za ndani, itue Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 7:00 usiku saa za ndani na katizo la safari la saa moja mjini Dar es Salaam.

    FZ671 imepangiwa kuondoka Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 12:40 asubuhi saa za ndani, iwasili Uwanja wa Ndege wa Unguja saa 7:05 mchana saa za ndani na katizo la safari la saa moja mjini Dar es Salaam.

    Nauli za safari ya pande mbili

    Nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Uchumi kutoka Unguja hadi Dubai itaanzia Dola 399 za Marekani ikijumuisha mzigo wa 20kg uliokaguliwa, huku nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Biashara itaanzia Dola 1499 za Marekani na inajumuisha kodi zote na mzigo wa 40kg uliokaguliwa. Hizi ni nauli maalum za uzinduzi za mwezi mmoja.

    Tiketi za safari hizo za ndege zinaweza kununuliwa kuanzia leo kutoka tovuti ya flydubai (flydubai.com), Kituo chake cha Simu cha ndani +255 (22) 2124005, maduka ya usafiri ya flydubai au kupitia wabia wa usafiri. Taarifa na maelezo zaidi ya huduma za shirika hili za ukodishaji gari na bima ya safirini pia zinaweza kupatikana kwenye flydubai.com.

    Distributed by APO (African Press Organization) on behalf of flydubai.

    Media contact:

    Houda Al Kaissi

    Senior Press Officer

    t. +971 4 603 3073

    m. +971 56 683 0336

    news@flydubai.com

    Kuhusu flydubai:

    Shirika la ndege lenye makao yake Dubai linajikakamua kuondoa vizuizi vya usafiri na kuimarisha uhusiano kati ya tamaduni tofauti katika mtandao wake unao endelea kukua. Tanug uzinduzi wa biashara yake mnamo 2009, flydubai (http://www.flydubai.com):

    • Imeunda mtandao wa vituo 83, pamoja na safari 20 mpya zilitangazwa 2014.

    • Imefungua safari 53 mpya ambazo hapo awali hazikuwa na safari za moja kwa moja hadi Dubai au hazikuwa zinahudumiwa na shirika la kitaifa la Umoja wa Falme za Kiarabu kutoka Dubai.

    • Imeunda msafara wa ndege 40 mpya na inasubiri kuwasilishwa kwa zaidi ya ndege 100 ifikapo mwisho wa 2023.

    Zaidi ya hayo, wepesi na urahisi wa flydubai kama shirika changa la ndege umeimarisha ukuaji wa uchumi wa Dubai, kufuatana na dira ya Serikali ya Dubai, kwa kuanzisha mtiririko wa biashara na utalii katika masoko ambayo hayakuwa na huduma hizi.

    For more information about flydubai services, please visit http://www.flydubai.com.

    Support InfoStride News' Credible Journalism: Only credible journalism can guarantee a fair, accountable and transparent society, including democracy and government. It involves a lot of efforts and money. We need your support. Click here to Donate

    African News African Press Release APO News East Africa Eastern Africa
    Share. Facebook Twitter WhatsApp Pinterest Reddit Tumblr VKontakte Email LinkedIn

    Related Posts

    Africans Coming Together As One Is The Only Way Forward – Burna Boy

    Mar 21, 2023

    Morocco Has Made Africa Proud – Coach

    Dec 11, 2022

    Senegal’s Togetherness Is Unmatched – Koulibaly

    Nov 30, 2022

    It Is Refreshing To See African Teams With African Managers In Qatar – Oliseh

    Nov 25, 2022
    Add A Comment

    Comments are closed.

    Get Social with Us
    • Facebook
    • Twitter 6.5K
    • Pinterest 92
    • Instagram
    • YouTube
    Latest Posts

    Larissa London Celebrates Her Son With Davido On His Birthday

    Mar 25, 2023

    I’m Grateful To My Coaching Staff For Always Being Available To Work With Me – Tuchel

    Mar 25, 2023

    I Wonder Why Women Still Get Deceived By Unverified Accounts – Frederick Leonard

    Mar 25, 2023

    I Was Loooking Forward To Seeing Rashford – Gareth Southgate

    Mar 25, 2023

    Subscribe to Updates

    Get the latest breaking news straight into your inbox!

    Random News

    I Support Buhari – Ben Ayade

    Aug 27, 2016

    Top UN official in West Africa urges end to ‘unprecedented' spate of violence in Nigeria

    Mar 5, 2014

    Maitama Sule Believed In Nigeria’s Unity – GEJ

    Jul 10, 2017

    Senate Clears Shekarau, 3 Others As Ministers

    Jul 3, 2014

    InfoStride News delivers the latest breaking news, Nigeria news, world news and top stories on business, celebrity, entertainment, politics, sports, technology and more. Experience the best of in-depth coverage, special reports, football highlights, political opinions, crime watch, celebrity gossips etc.

    GooglePlay Store Button

    Support InfoStride News' Credible Journalism

    Credible journalism involves a lot of efforts and money; and can guarantee a fair, accountable and transparent society, including democracy and government. We need your support to continue offering free access to our loyal readers and visitors like you.

    Click here to Donate

    Facebook Twitter Instagram Pinterest YouTube Tumblr LinkedIn RSS
    • Our Terms
    © 2023 InfoStride News. All Rights Reserved.

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.

    Sign In or Register

    Welcome Back!

    Login to your account below.

    Continue with Facebook
    Continue with Google
    Continue with Twitter
    Lost password?